Star Tv

Watawala wa kijeshi wa Sudan na viongozi wa maandamano wameanza tena leo mazungumzo juu ya kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia baada ya siku kadhaa za mkwamo katika majadiliano. Viongozi wa maandamano Omar al-Digeir na Satea al-Haj ni miongoni mwa wanaohudhuria mazungumzo hayo kwa niaba ya vuguvugu la Allance for Freedom and Change.

Mkutano huo wa faragha unaandaliwa katika jumba la mikutano katikati ya mji mkuu Khartoum. Duru hii mpya ya mazungumzo imekuja wakati maelfu ya waandamanaji wakiendelea kupiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi katikati ya Khartoum. Makamanda wa kijeshi na waandamanaji wanatofautiana kuhusu ni nani atakayeshirikishwa katika serikali ya mpito itakayochukua nafasi ya baraza la sasa la kijeshi. Wakuu wa jeshi wanapendekeza kuwa baraza jipya la mpito liongozwe na jeshi, wakati viongozi wa maandamano wanataka liendeshwe kwa kiasi kikubwa na raia.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.