Star Tv

Rais wa Rwanda Paul Kagame amefanya mazungumzo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika ziara yake ya kwanza katika nchi jirani baada ya mvutano wa mwaka 2019 na kusababisha kufungwa kwa mpaka wa nchi hizo mbili kwa miaka mitatu.

Taarifa kutoka Ikulu ya Entebbe imesema viongozi hao wawili wamekubaliana kutoa kipaumbele kwa amani na utulivu katika eneo hilo kwa kushughulikia mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Museveni ameutaka umoja wa kikanda kushughulikia ukosefu wa usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kabla ya mzozo huo kuongezeka.

Kagame amesema ni muhimu pande zote katika mzozo huo zishirikishwe ili kutatua mgogoro huo mara moja.

Rais Kagame alikuwa katika ziara ya faragha nchini humo kuhudhuria dhifa ya mtoto wa Museveni ambaye pia ni kamanda wa kikosi cha nchi kavu cha Uganda Lt. Jenerali Muhoozi Kainerugaba, aliyesherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 48 mwishoni mwa juma.
#ChanzoBBC

Latest News

Dkt. Jafo ofisi yake, imekamilisha taratibu zote za kupata Ithibati ya Kitabu ch...
24 Apr 2023 09:38 - Kisali Shombe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasilisha bungeni Hotuba ya Ma [ ... ]

TARI, Ukiruguru kuzindua Kifaa cha kupandia Mbegu cha Rafiki
23 Apr 2023 18:33 - Kisali Shombe

Sekta ya Kilimo ni mhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia Pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa uj [ ... ]

Wanawake kuwa sehemu ya Elimu dhidi ya Itikadi Kali na Ugaidi Afrika.
17 Apr 2023 10:28 - Kisali Shombe

Mnamo Oktoba 14, 2017, Mogadishu, Somalia ilikumbwa na shambulio baya la kigaidi lililoua watu 587 na kujeruhi zaidi ya  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.