Star Tv

Takriban Wanyarwanda 100 ambao walikimbilia kisiwa kilichopo Ziwa Kivu katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kuepuka kupata chanjo za Covid wamerudishwa nchini kwao.

Hata hIvyo watu wawili wanadaiwa kutoonekana katika kundi hilo la Wanyarwanda 101 huku operesheni ya kuwasaka inaendelea.

Afisa wa Kisiwa cha Idjwi, Roger Ntambuka, aliiambia BBC kwamba mamlaka iliweza kufanya mazungumzo na Wanyarwanda hao ili kuwarejea nyumbani kwao.

"Hakukuwa na sababu ya Wanyarwanda hawa kubaki hapa. Tuliweza kuwashawishi,"-Amesema.

Amesema raia hao wa Rwanda, ambao ni wanawake, wanaume na watoto, waliondoka kuelekea nyumbani kwa boti.

Gavana wa jimbo la magharibi mwa Rwanda amesema hakuwa na habari kuhusu Wanyarwanda waliokimbia na haijabainika kama mamlaka ilihusika katika kuwarejesha nchini kwao.

Wiki iliyopita mamlaka ya Burundi iliwafukuza zaidi ya Wanyarwanda 10 waliokuwa wameingia nchini humo kukwepa chanjo ya lazima ya corona na kuwarudisha nyumbani.

Raia wa Rwanda lazima wapewe chanjo ili kuruhusiwa kutumia usafiri wa umma, kwenda kwenye maeneo ya starehe (bar) na migahawa au kuhudhuria hafla za umma.

#ChanzoBBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.