Star Tv

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa tarehe 24 Disemba mwaka huu.

Tume ya uchaguzi ilikataa maombi kadhaa ya kugombea kiti hicho akiwemo Saif al-Islam Gaddafi, ikitaja "sababu za kisheria", vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Bwana Saif al-Islam Gaddafi aliibua utata baada ya kutangaza kwamba atagombea urais.
Anasakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa madai ya uhalifu wa kivita na mauaji wakati baba yake alipoongoza taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika.

Maombi ya mwanasiasa mwenye ushawishi Khalfa Haftar pia yalisababisha wasiwasi katika nchi hiyo kwani anakabiliwa na mashitaka katika mahakama za Marekani, lakini haijawa wazi iwapo yuko miongoni mwa wale ambao wamekuwa wakikataliwa.

Waendesha mashitaka wa kijeshi wa Libya walikuwa wameiomba tume ya uchaguzi kuzuwia mchakato wa makaratasi ya kugombea kwa Bwana Gaddafi na Bwana Haftar hadi watakapojibu maswali juu ya shutuma dhidi yao.

Watu sitini waliwasilisha maombi ya kugombea urais wa Libya mpaka kufikia siku ya Jumatatu.
#ChanzoBBC

 

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.