Star Tv

Serikali ya Nigeria katika jimbo la Kwara imesema imemsimamisha mkuu wa shule ya Quran katika jimbo hilo baada ya video kusambaa ikionesha makundi ya wanafunzi wakiwa wanaadhibiwa na wenzao kwa kutokuwa na nidhamu.

Baadhi ya wanafunzi hao ambao walikuwa wa kike na kiume walishutumiwa kunywa pombe katika sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa mwanafunzi mwenzao.

Ingawa, wanafunzi hao wanadai kuwa walikunywa maziwa ya mtindi tu.

Hata hivyo waliendelea kupigwa na wanafunzi wenzao ambao walikuwa wanapewa amri na mwalimu wa Quran.

Video moja ambayo ilisambaa mitandaoni na kuonekana na BBC, inawaonesha wanafunzi wa kike wakiwa wamepiga magoti wakati wakipigwa fimbo na wanafunzi wa kiume na wengine wakiwa wanatazama.

Kamishna wa elimu na maendeleo alitoa taarifa Jumapili na kusema wanafunzi hao wamepelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa kiafya na matibabu.

Taarifa ya serikali inayotaka uchunguzi ufanyike dhidi ya tukio hilo na adhabu kali zinazotolewa shuleni.

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.