Star Tv

Kikundi cha waasi cha eneo la Tigray, Ethiopia kimesema kuwa watu 150 wamekufa kutokana na njaa na kukosekana kwa misaada ya kibinadamu kunafanya hali kuwa mbaya zaidi.

Serikali ya Ethiopia haijajibu lolote kuhusu madai hayo. Lakini awali ilikanusha madai ya Umoja wa Mataifa kuhusu kuweka zuio la misaada kuingia.

Mkuu wa kilimo wa TPLF, Atinkut Mezgebo alisema watu na wanyama wanakufa kutokana na kukosa chakula na dawa na "janga linaweza kuwa kubwa zaidi ya tujuavyo".

Aliiambia BBC Tigrinya kuwa watu wanakufa kutokana na njaa huku wanawake na watoto wakiwa ndio waathirika wakubwa zaidi wa uhaba wa chakula.

Si rahisi kuhakiki madai haya kwa kuwa bado mawasiliano ya simu yamekatwa na intaneti haifanyi kazi Tigray.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la Tigrayan siku ya Jumatatu, imesema kuwa kuna baadhi ya vifo vinavyotokea katika kambi na watu kuhama makazi kutokana na mgogoro unaoendelea.

Kwa mujibu wa UN, malori 100 ya chakula yanapaswa kuingia katika eneo hilo kila siku ili kukidhi misaada ya kibinadamu.

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.