Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka tena kusitishwa mapigano mara moja katika eneo la Ethiopia la Tigray, ambapo vikosi vya serikali na wapiganaji waasi wamekuwa katika mizozo tangu Novemba mwaka jana.
António Guterres alielezea hali ya kibinadamu huko Tigray kama "mbaya" na akasema mashirika ya misaada yanahitaji kufika katika eneo hilo bila vikwazo.
"Mazungumzo kama haya yanaweza kuchangia kushughulikia sababu za msingi za mzozo na kuhakikisha sauti za Waethiopia zinaleta njia ya amani," alisema.
Tangu kuanza kwa mapigano katika jimbo hilo mamilioni ya watu wamehama makazi yao na mamia ya maelfu wanaishi katika hali ya njaa.
#ChanzoBBCSwahili