Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi amesema hali sio nzuri lakini ipo katika udhibiti baada ya kuripuka kwa volcano katika eneo Goma huko mashariki mwa taifa hilo.

Akizungumza baada ya serikali yake kutangaza kwa makosa kutokea mlipuko mwingine wa volkano, ikiwa ni takribani juma moja baada ya mlipuko wa Mlima Nyiragongo.

Rais Tshisekedi ameonya kwa kusema kwa hali ilivyo mripuko unaweza kutokea kokote katika jiji la Goma kwa kuwataka wakazi wa mji huo kutoharakisha kurejea katika makazi yao.

Taarifa yake hiyo anaitoa baada ya kuwepo kwa ripoti zinazosema zaidi ya wakimbizi 1,000 wameondoka katika kambi walizokuwa wanahifadhiwa huko Rwanda kurejea Goma.

Takribani wakazi 400,000 waliokolewa katika eneo la mashariki la Goma, baada ya wiki moja ya matetemeko ya ardhi, yalitokana na mripuko wa moja ya vokano hai barani Afrika.

Latest News

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KULIPA KODI BILA KUCHOKA.
14 Jun 2021 19:01 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kujitoa kulipa kodi ili kuwez [ ... ]

WAZIRI MKUU MPYA AAPA KUIUNGANISHA ISRAEL.
14 Jun 2021 06:33 - Grace Melleor

Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo ambalo linalezwa kufadhaishwa na chaguzi nne  [ ... ]

RAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NA JENGO LA BOT.
13 Jun 2021 14:11 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza kinach [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.