Star Tv

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekana mashitaka ya ufisadi yaliyokuwa yakimkabili mwanzoni mwa kesi yake katika mahakama ya Pietermaritzburg.

Kiongozi huyo ambaye wakati mmoja aliwahi kusherehekewa kwa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi anatarajiwa kukana mashitaka ya udanganyifu na ulaghai katika kesi ambayo ilianza na mkataba wa silaha miaka ya 1990.

Zuma alidai kuwa yeye ni “mwathiriwa wa hujuma za kisiasa na kwamba mahakama nchini humo zinashirikiana na mahasimu wake wa kisiasa”.

Bwana Zuma pia anakabiliwa na madai mapya ya ufisadi na huenda akafungwa jela kwa kukiuka amri ya mahakama katika kesi nyingine tofauti.

Baadhi ya mashujaa wa ukombozi wa Afrika Kusini wamemshtumu Zuma huku wakimlinganisha na ‘jambazi na kuonya itachukua muda mrefu kurekebisha uharibifu’ alioufanya dhidi ya taasisi changa za nchi hiyo.
Chanzo:BBCSwahili

Latest News

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KULIPA KODI BILA KUCHOKA.
14 Jun 2021 19:01 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kujitoa kulipa kodi ili kuwez [ ... ]

WAZIRI MKUU MPYA AAPA KUIUNGANISHA ISRAEL.
14 Jun 2021 06:33 - Grace Melleor

Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo ambalo linalezwa kufadhaishwa na chaguzi nne  [ ... ]

RAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NA JENGO LA BOT.
13 Jun 2021 14:11 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza kinach [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.