Star Tv

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amewafuta kazi Wakuu wa majeshi, Ambao ni Jeshi la ardhini na angani.

Rais Nyusi amefikia hatua hiyo wakati nchi hiyo inapokabiliana na wanamgambo wa Islamic States Kaskazini na waasi wa wanamgambo wanaohusishwa na chama kikuu cha upinzani.

Katika taarifa iliyotolewa usiku Alhamisi rais hakutoa sababu ya kumfuta kazi Ezequiel Isac Muianga, Mkuu wa jeshi la ardhini, na Messias André Niposso, mkuu wa jeshi la anga.

Rais pia amemfuta kazi Kamanda na Naibu Kamanda wa chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Marechal Samora Macheya.

Aidha Naibu Kamanda wa Taasisi ya mafunzo ya juu ya masuala ya ulinzi nchini humo pia amefutwa kazi.

Latest News

RAIS TSHISEKEDI ADHIBITI BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI.
13 Apr 2021 18:22 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alitangaza baraza jipya la Mawaziri katika hatua ambayo inaimar [ ... ]

MALIPO YA NDEGE MPYA TATU YAKAMILIKA.
13 Apr 2021 18:04 - Grace Melleor


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema tayari serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu.

WASAFIRI KUTOKA KENYA KUINGIA KARANTINI KWANZA IRELAND.
12 Apr 2021 13:43 - Grace Melleor

Wasafiri wanaoelekea Ireland kutoka Kenya watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya ba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.