Star Tv

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis anayeendelea na ziara yake ya kihistoria nchini Iraq ametoa wito kwa viongozi na watu wa nchi hiyo kuepuka vurugu na mivutano ya kidini.

Papa Francis anafanya ziara ya siku nne nchini Iraq ambayo ni ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Kanisa Katoliki kwenye taifa hilo la Mashariki ya Kati.

Usalama umeimarishwa kwa ajili ya kumlinda kiongozi huyo wa kanisa katoliki baada yakutokea mashambulio ya roketi na yale ya kujitoa muhanga katika siku za hivi karibuni nchini humo.

Wakati huo huo hatua za kiafya zinazingatiwa zaidi kutokana na hali ya maambukizi ya virusi vya corona yanayoongezeka nchini Iraq.

Baba mtakatifu atakutana na kiongozi wa madhehebu ya Shia nchini Iraq, Ayatollah Ali Sistani pamoja na pia atazuru miji minne ukiwemo mji wa Mosul ambako makanisa na turathi nyingine zimeharibiwa na wanamgambo wa itikadi kali.

Latest News

RAIS TSHISEKEDI ADHIBITI BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI.
13 Apr 2021 18:22 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alitangaza baraza jipya la Mawaziri katika hatua ambayo inaimar [ ... ]

MALIPO YA NDEGE MPYA TATU YAKAMILIKA.
13 Apr 2021 18:04 - Grace Melleor


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema tayari serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu.

WASAFIRI KUTOKA KENYA KUINGIA KARANTINI KWANZA IRELAND.
12 Apr 2021 13:43 - Grace Melleor

Wasafiri wanaoelekea Ireland kutoka Kenya watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya ba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.