Star Tv

Idadi isiyofahamika ya mamba wadogo hawajulikani walipo baada ya kutoroka katika shamba wanapofugwa eneo la Cape Magharibi Afrika Kusini Jumatano, kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo.

Juhudi za kutafuta mamba hao kila mmoja akiwa na urefu wa zaidi ya mita moja zinaendelea.

Aidha, inashukiwa kwamba huenda wamepata njia inayowapeleka kwenye mto Breede ulio karibu.

"Ni hatari kiasi fulani kwa jamii kwasababu wamekuwa wakifungwa na wamezoea chakula cha kawaida, hawajitafutii chakula".

Msemaji wa serikali eneo hilo James-Brent Styan pia amenukuliwa na gazeti la Times Live akisema kuwa wanyama hao ni hatari kama wengine wowote wale wa aina hiyo ambao ni hatari kwa binadamu.

Takribani mamba 20 wamerejeshwa katika shamba wanapofugwa, kulingana na afisa wa eneo aliyenukuliwa na Tovuti ya Eye Witness News.

Chanzo: BBC Swahili

Latest News

RAIS TSHISEKEDI ADHIBITI BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI.
13 Apr 2021 18:22 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alitangaza baraza jipya la Mawaziri katika hatua ambayo inaimar [ ... ]

MALIPO YA NDEGE MPYA TATU YAKAMILIKA.
13 Apr 2021 18:04 - Grace Melleor


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema tayari serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu.

WASAFIRI KUTOKA KENYA KUINGIA KARANTINI KWANZA IRELAND.
12 Apr 2021 13:43 - Grace Melleor

Wasafiri wanaoelekea Ireland kutoka Kenya watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya ba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.