Star Tv

Jeshi la UPDF na polisi nchini Uganda wamewaruhusu wanasheria wa waliokuwa wa mgombea wa kiti cha urais Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine kumtembelea nyumbani kwake Magere anakozuiwa na vikosi hivyo kwa zaidi ya juma moja.

Hii ni baada ya mahakama kuu jana kutoa maamuzi ya ombi la Kyagulanyi na mkewe la kuondolewa kwa vikosi vya jeshi na polisi nyumbani kwake.

Kulingana na mwandishi wa BBC Issaac Mumena, mawakili hao waliruhusiwa kumuona baada ya kukaguliwa kwenye kizuizi cha jeshi kilichowekwa karibu na nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa Asumani Basalirwa aliyezungumuza na BBC kwa njia ya simu, iliwachukua muda wa saa kadhaa kuwashawishi wakuu wa jeshi la UPDF na polisi kuweza kumuona mteja wao, lakini baadhi ya watu waliokwenda nao walibaki kwenye kizuizi cha jeshi akiwemo aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais Jenerali Henry Tumukunde.

Mwanasheria Basalirwa ameeleza kuwa wamemkuta Bobi Wine akiwa na upungufu wa chakula kutokana na kumzuia kutotoka nje na pia kuwazuia watu kuingia nyumbani kwake ambao wangemletea chakula lakini hali yake kiafya sio mbaya.

“Afya yake ni nzuri, hakuna kitu chochote lakini yeye anataka kitu kimoja tu nacho ni haki yake, anataka apewe uhuru kutoka kwake nyumbani kwenda kufanya kazi yake arudi’’- amesema Asumani Basalirwa.

Masuala muhimu yaliyowapeleka wanasheria hao kwa kiongozi wa chama cha NUP ni pamoja na kushauriana naye jinsi ya kuwasilisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 14 mwezi huu wa Januari, yaliyompatia Rais Museveni ushindi wa kuongoza muhula wa sita.

Chanzo na BBC Swahili.

 

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.