Star Tv

Umoja wa Ulaya (EU) umesema ina wasiwasi juu ya wanasiasa pamoja na washika dau wa mashirika ya kiraia wanavyonyanyaswa nchini Uganda.

Taarifa kutoka kwa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Ulaya imesema vitendo vya vikosi vya usalama ambavyo havikubaliki vilisababisha vurugu kabla ya uchaguzi.

Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa serikali ya Uganda kuzuia vikosi vyake vya usalama, kuchunguza unyanyasaji na kuwajibisha wote waliokiuka hatia.

Wakati huohuo, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa mamlaka za Uganda kuagiza polisi na wanajeshi wake kuondoka mara moja katika makazi ya mgombea wa upinzani Bobi Wine ambayo wamekuwa wakiyazingira na kumzuia Bobi Wine pamoja na mke wake Barbara Itungo Kyagulanyi kutotoka nje.

Shirika la Amnesty International limesema ikiwa ni siku saba tangu Bobi Wine na mke wake wazuiliwe kutoka nje ya makazi yao; "Huku ni kukamata watu kiholela’’.

Robert Kyagulanyi na mke wake Barbara wamewekewa kifungo cha nyumbani bila kujulishwa makosa yao wala kufikishwa mahakamani.

"Kuzuiwa kwake kumefanya iwe changamoto kwa Bobi Wine kupinga matokeo ya uchaguzi katika kile ambacho kimejitokeza kuwa njama za kukizuia chama cha NUP kufika mahakamani kwa wakati”- amesema Deprose Muchena, Mkurugenzi wa Amnesty International eneo la Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Polisi wamekuwa wakimzuia Bobi Wine kuondoka nyumbani kwake tangu Ijumaa baada ya kuanza kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Januari 14.

Rais Yoweri Museveni alitangazwa mshindi baada ya kuibuka na asilimia 58.64 ya kura zilizopigwa huku Bobi Wine ambaye ndio mpinzani wake mkuu akipata asilimia 34.83 ya kura.

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.