Umoja wa Mataifa na serikali katika Jamhuri ya Afrika ya kati (CAR) wamesema waasi nchini humo wamefanya mashambulio mawili karibu na mji mkuu wa Bangui.
Taarifa kutoka nchini humo zinasema shambulio moja lililenga kituo cha ukaguzi kinachodhibitiwa na wanajeshi wa serikali na mamluki wa Urusi.
Mawaziri wanasema kuwa washambuliaji walirudishwa nyuma, lakini msemaji wa Umoja wa Mataifa ameelezea mapigano kama yanayoendea.
Ubalozi wa Marekani unasema kuwa umepokea taarifa za makabiliano katika mji wa Bungui na katika eneo la Bimbo kuelekea magharibi mwake
Vikosi vya waasi, vilivyopinga kuchaguliwa tena kwa Faustin-Archange Touadéra na vilimuunga mkono rais wa zamani François Bozizé,wamekuwa wakisonga mbele kuelekea katika mji mkuu.