Star Tv

Kampuni ya mafuta ya Total imewaondoa maelfu ya wafanyakazi wake katika visima vya mafuta vilivyopo Kaskazini mwa Msumbiji.

Kampuni hiyo imefikia hatua hiyo baada ya wanamgambo walio watiifu kwa kundi la Islamic State kutishia kushambulia mji muhimu katika eneo hilo.

Vyombo vya habari vinasema kwamba Wanamgambo hao walisambaza vijikaratasi vinavyotishia kushambulia eneo la Palma katika mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Cabo Delgado.

Tishio hilo lilisababisha Total kuwaondoa wafanyakazi wake katika eneo la Afunsi karibu na Palma ambapo linaongoza ujenzi wa kiwanda cha gesi chenye thamani ya $14.9bn.

Mtandao wa Carta de Mocambique umesema kwamba wapiganaji hao walikabiliana na vikosi vya serikalikaribu na palma tarehe mosi Januari.

Mkoa wa Cabo Delgado, ambapo ni nyumbani kwa rais Fillipe Nyusi , unapakana na Tanzania na umekumbwa na ghasia mbaya zilizotekelezwa na wapiganaji hao tangu 2017.

Latest News

WANAOGESHA MAGARI BARABARANI HOVYO KUWAJIBISHWA BILA HURUMA.
20 Jan 2021 14:26 - Grace Melleor

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ameitaka Bodi ya mfuko wa Barabara (RfB) kutumia vifungu [ ... ]

KENYA KUPOKEA DOZI MILIONI 24 ZA CHANJO YA CORONA.
20 Jan 2021 14:06 - Grace Melleor

Kenya inatarajia kupokea dozi milioni 24 za chanjo ya ugonjwa corona iliyotengenezwa na kapuni ya Astrazeneca na chuo ki [ ... ]

BIDEN AJIANDAA KUINGIA IKULU, HUKU TRUMP AKISUSIA KUHUDHURIA KUAPISHWA KWAKE.
20 Jan 2021 08:14 - Grace Melleor

Rais mteule wa Marekani Joe Biden aliwasili Washington katika mkesha wa sherehe ya kuapishwa kwake, wakati mtangulizi wa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.