Star Tv

Umoja wa Mataifa umesema kuwa umefanikiwa kuukomboa mji wa Bambari nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao ulikuwa umetekwa na waasi siku ya Jumanne.

Taarifa kutoka nchini humo zimebaibisha kuwa raia waliyokuwa wametoroka mji huo baada ya mapigano kuzuka wameanza kurejea nyumbani, Ambapo nchi hiyo inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu Jumapili hii.

Serikali imemlaumu rais wa zamani François Bozizé, kwa kuunganisha makundi yaliyojihami katika jaribio la kufanya mapinduzi - madai ambayo amekanusha.

Urusi na Rwanda zimepeleka mamia zaidi ya wanajeshi kusaidia serikali, huku waasi wakijaribu kuelekea mji mkuu wa Bangui.

Urusi imetuma askari wa ziada 300 wa mafunzo katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kukabiliana na kile Wizara ya mashauri ya kigeni ya nchi hiyo imesema "kushuka kwa kiwango cha usalama kwa hali ya juu ".

Takriban wanajeshi 750 wa Rwanda na maafisa wa polisi wamekuwa wakifanyia kazi nchini humo chini ya kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa kinachojulikana kama Minusca.

Rwanda imepeleka kile inachokiiya "kikosi cha ulinzi " katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati baada ya walinzi wake wa amani kushambuliwa na waasi katika mji mkuu, Bangui.

Rais wa Rwanda Paul Kagame alisema kwamba nchi yake iliamua kutuma askari katika Jamuhuri ya Afrika ya kati ili kulinda askari wa nchi hiyo waliomo katika kikosi cha umoja wa mataifa ambao wamekuwa wakilengwa na wanamgambo wenye silaha.

Rais Faustin Archange Touadéra amesisitiza kuwa uchaguzi wa Jumapili utaendelea kama ulivyopangwa, akisema kuwa uwepo wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa unamaanisha kuwa watu hawana la kuogopa.

Lakini vyama vya kisiasa vya upinzani, kikiwemo cha Bw Mr Bozizé, vimetoa wito wa kuahirishwa kwa uchaguzi "hadi amani na usalama vitakapopatikana ".

Makundi ya waasi yamechukua udhibiti wa miji kadhaa iliyopo karibu na mji mkuu Bangui, huku wakikabiliana na vikosi vya usalama na kupora mali, na Umoja wa Mataifa umesema kuwa wanajeshi wake wanafanya hima kule amani Bangui.

Chanzo na BBC Swahili.

Latest News

WANAOGESHA MAGARI BARABARANI HOVYO KUWAJIBISHWA BILA HURUMA.
20 Jan 2021 14:26 - Grace Melleor

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ameitaka Bodi ya mfuko wa Barabara (RfB) kutumia vifungu [ ... ]

KENYA KUPOKEA DOZI MILIONI 24 ZA CHANJO YA CORONA.
20 Jan 2021 14:06 - Grace Melleor

Kenya inatarajia kupokea dozi milioni 24 za chanjo ya ugonjwa corona iliyotengenezwa na kapuni ya Astrazeneca na chuo ki [ ... ]

BIDEN AJIANDAA KUINGIA IKULU, HUKU TRUMP AKISUSIA KUHUDHURIA KUAPISHWA KWAKE.
20 Jan 2021 08:14 - Grace Melleor

Rais mteule wa Marekani Joe Biden aliwasili Washington katika mkesha wa sherehe ya kuapishwa kwake, wakati mtangulizi wa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.