Kundi la kigaidi la Boko Haram limesema lilihusika na utekaji nyara wa mamia ya wavulana wa shule katika jimbo la Kaskazini-Magharibi la Katsina State nchini Nigeria.
Kundi hilo limetoa taarifa hiyo huku likigusia jinsi lilivyoendelea kutekeleza mashambulio hatari katika wiki za hivi karibuni, Tovuti kibinafsi ya Daily Nigerian limeripoti.
Mamia ya wavulana wa shule ya upili ya serikali iliyopo Kankara katika jimbo la Katsina hawajulikani kufuatia shambulio hilo la Ijuma usiku wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa Daily Nigerian, kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, alisema hayo katika ujumbe wa dakika nne uliyorekodiwa na kundi lililotekeleza shambulio hilo.
"Kilichofanyika Katsina hi hatua ya kunadi Uslamuna kupingaelimu inayoenda kinyume na mafundisho Kiislamu kwani elimu ya magharibi hairuhusiwi na Allah na Mtume wake mtakatifu," tovuti hiyo ilimnukuu Shekau akisema.
Tovuti hiyo imearifu kuwa Shekau hakutoa maelezo kuhusu shambulio hilo, idadi ya wanafunzi waliotekwa au kuthibitisha ripoti kuhusu majadiliano na serikali.