Star Tv

Zaidi ya wabunge 200 kati ya wabunge 500 wameanza kikao cha kupiga kura ya kutaka kumuondoa madarakani Spika wa bunge Jeanine Mabunda kutoka chama cha Joseph kabila.

Wabunge wa upande wa rais aliyeko madarakani Felix Tschisekedi wanamtuhumu kwa uongozi mbaya.

Kwa mujibu wa mbunge Moindo Nzangu, ambaye aliwasilisha mapendekezo ya kura hiyo mwanzilishi Spika Bi Jeanine Mabunda atatakiwa kujitetea mbele ya wabunge kabla ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Kikao hicho ambacho kilipangwa kuanza saa nne asubuhi kimechelewa kutokana na msako na ulinzi mkali uliofanywa na vikosi vya usalama ndani ya bunge.

Vurugu na ghasia zilitokea ndani ya bunge hilo wiki hii wakati ulipowasilishwa muswada wa kura ya maoni na watu kadhaa walijeruhiwa wakati wanaharakati na wabunge walipoanza kurushiana viti na kuharibu samani ndani ya bunge.

Mzozo wa hivi karibuni wa kisisia nchini Congo umeibuka tena baada ya rais Félix tshikedi kutangaza nia yake ya kuvunja bunge ili apate wingi wa wabunge ambalo kwa sasa lina idadi kubwa zaidi ya wabunge kutoka chama cha mtangulizi wake rais mstaafu Joseph Kabila.

Mzozo wa kisiasa uliibuka baada ya Félix Tshisekedi kutangaza mpango wa kuvunja serikali ya muungano na wafuasi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Joseph Kabila.

Jumapili Rais wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi, alitangaza kuweka mpango wa kuvunja serikali ya muungano na wafuasi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Joseph Kabila.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.