Star Tv

Makabiliano yametokea baada ya Rais Tschisekedi kutangaza kuwa anataka kufanya mageuzi.

Kumekuwa na makabiliano makali ndani ya Bunge la taifa katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kati ya wanaharakati wa chama cha kabila na chama chaRais Felix Tshikedi.

Taarifa zimeeleza kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa katika makabiliano hayo.

Kundi la wanaharakati wa chama cha rais mstaafu Joseph Kabila walikuja kuzuia kikao cha wabunge ambao wanataka spika wa bunge aondolewe.

Picha za video zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha watu wakirushiana viti na kuharibu baadhi ya vifaa ndani ya bunge hilo lililopo mjini Kinshasa, huku polisi wakiwakimbiza.

Mzozo uliibuka wakati wabunge wanaomuunga mkono Rais Felix Tshikedi katika nia yake na kuanza kuwashawishi wabunge ili apate idadi kubwa ya wabunge kabla ya kuunda serikali yake mpya.

Kundi hilo la wawakilishi wa raia walikuja kuwasilisha, kura zao za maoni jana za kutaka Spika wa bunge Bi Jeanine Mabunda ambae ni mwanachama wa chama cha Bw Kabila aondolowe wakimtuhumu kuongoza bunge vibaya, lakini Spika wa bunge hakuwepo bungeni.

Rais Tshisekedi alitangaza siku ya Jumapili kwamba mpango wake wa mageuzi unawekewa pingamizi na alitaka kuunda serikali mpya ya muungano au kutangaza uchaguzi upya.

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.