Star Tv

Mgombea wa urais nchini Uganda Robert Kyagulanyi, anayefahamika zaidi kama Bobi Wine ameahirisha kampeni zake.

Sababu za mgombea huyo wa urais kuahirisha kufanya kampeni zake ni kufuatia kujeruhiwa kwa maafisa wake wa kampeni na kuharibiwa kwa gari lake.

Kiongozi huyo wa upinzani anasema risasi zilifyatuliwa kwenye gari lake na kutoboa matairi ya gari lake na kumfanya asiweze kusafiri tena.

Video zilizosambazwa na timu yake ya kampeni kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha kitu ambacho hakikutambuliwa kikilipuka umbali wa mita kadhaa kutoka mahali alipokuwa.

Awali katika eneo la Kayunga, mashariki mwa Kampala, gesi za kutoa machozi zilitumika kuwatawanya wafuasi wake.

Maafisa wanne wa kampeni yake walijeruhiwa Mmoja wao, aliyetambuliwa kama producer Dan Magic alipigwa usoni.

Mmoja wa polisi wanaowalinda wagombea wa urais waliotolewa na Tume ya Uchaguzi pia alijeruhiwa.

Takribani wiki mbili zilizopita, watu 54 waliuawa wakati wafuasi wa mgombea huyo walipokuwa wakiandamana kudai aachiliwe huru baada ya kukamatwa na polisi katika mkutano wa kampeni.

 

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.