Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema ameanzisha "awamu ya mwisho" ya operesheni ya kijeshi katika jimbo la Tigray kwanza kushambulia mji mkuu wa jimbo hilo, Mekelle.
Waziri Abiy amesema wanajeshi watajaribu wasiwajeruhi raia na ametoa wito kwa watu katika mji huo kusalia majumbani mwao.
Hatua hilo inajiri baada ya muda wa mwisho uliyotolewa kwa wapiganaji wa Tigray kujisalimisha kumalizika siku ya Jumatano.
Chama cha TPLF, ambacho kinadhibiti mji wa Mekelle, kimeapa kuendelea na mapigano.
Aidha, mamia ya watu wameripotiwa kuuawa na maelfu ya wengine kutoroka makwao huku vikosi vya muungano vya Ethiopia vikiteka miji kadhaa ya Tigray kutoka kwa wapiganaji wa TPLF.