Star Tv

Waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini, Bi Mapisa-Nqakula amekatwa mshahara wake na pesa hizo zitaelekezwa katika mfuko wa kukabiliana na virusi vya corona nchini humo.

Rais wa Afrika Kusini amemkata mshahara waziri wa ulinzi kwa miezi mitatu baada ya kuruhusu maafisa wa chama tawala kusafari kwa kutumia ndege ya jeshi hadi nchini Zimbambwe pamoja naye Septemba 9.

Nosiviwe Mapisa-Nqakula alishtumiwa kwa kuruhusu matumizi ya rasilimali ya taifa kwa sababu za siasa za chama.

Jeshi la nchi hiyo lilikuwa limeeleza kwamba waziri huyo alikuwa katika ziara rasmi ya kitaifa na kwamba aliwafanyia abiria wengine hisani kwa kuwabeba.

Bi. Mapisa-Nqakula alienda mji mkuu wa Zimbambwe, Harare kuhudhuria mkutano uliokuwa umepangiwa kujadili masuala ya kanda.

Ujumbe kutoka chama tawala cha Afrika Kusini - African National Congress (ANC) - ulikuwa unahudhuria mkutano huo kwa mazungumzo ya dharura na chama tawala cha Zimbambwe Zanu-PF lengo lao likiwa ni kutatua mgogoro wa kisiasa na kiuchumi nchini humo.

Lakini wasasiasa wa upinzani walimkosoa vikali waziri huyo kwa sababu aliandamana na ujumbe wa chama cha ANC.

Rais Ramaphosa, ambaye kipindi anaingia madarakani aliahidi kumaliza sifa mbaya ya chama cha ANC baada ya mwongo mmoja wa kashfa za ufisadi, alisema kwamba Waziri huyo kuandamana na wajumbe wa ANC kwa ndege aliyokuwa anatumia, hakufanya uamuzi stahiki unaozingatia uongozi mzuri.

Matokeo yake alisema ameamua kumkata mshahara Bi. Mapisa-Nqakula na pesa hizo zitaelekezwa katika mfuko wa kusaidia kukabiliana na janga la corona.

Wakati huo huo, chama cha upinzani cha Democratic Alliance kilisema hatua iliyochukuliwa na Bwana Ramaphosa haitoshi, Huku suala hilo huenda likajadiliwa zaidi bungeni huku kukiwa na wito wa waziri huyo kufutwa kazi.

Latest News

ETHIOPIA YASEMA HAITISHWI NA TAMKO LA RAIS DONALD TRUMP.
24 Oct 2020 16:54 - Grace Melleor

Waziri mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake "haitakubali vitisho vya aina yoyote" baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa M [ ... ]

RAIS TSHISEKEDI ATANGAZA MASHAURIANO YA UMOJA KWA MUUNGANO TAWALA.
24 Oct 2020 06:41 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, katika hotuba yake kwa taifa aliyoitoa siku ya Ijumaa wiki hi [ ... ]

SEKTA YA AFYA NCHINI YAPATA NEEMA KUTOKA USWISI.
23 Oct 2020 15:23 - Grace Melleor

Serikali imepokea msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 15.75 sawa na shilingi Bilioni 39.59 kwa ajili ya kugharamia mradi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.