Star Tv

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Add a comment

Wanawake wanaoishi vijijini huko Jamhumuri ya Kidemokrasi ya Kongo, hawana haki ya urithi wa mali pamoja na ardhi iliyoachwa na wazazi wao au waume zao. Na hii inatokana na mila na desturi zao zinazomtambua mwanaume kama mrithi pekee wa Ardhi.

Add a comment
Serikali ya Rwanda imeanza zoezi la kusajili upya wakimbizi kutoka Burundi miaka tatu tangu wakimbilie nchi humo. Usajili huo unafanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa, vifaa maalum vikinasa alama za macho na vidole.mwishowe kila mmoja atapatiwa kitambulisho cha kielectroniki chenye data zinazomhusu yeye na watu wa familia yake. Zoezi limeanzia mjini Kigali ambako kuna wakimbizi wanaokadiriwa kuwa elfu 30. Zoezi hilo linalodhaminiwa na shirika la umoja wa mataifa la wakimbizi linalenga kuwapa vitambulisho vya kielectroniki ili kuwa rahisishia kuishi maisha ya kawaida nchini Rwanda pamoja na kufanya kazi ama kuwa huru kutembea katika mataifa ya kigeni.Serikali pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wanasema usajili huu wa wakimbizi kutoka Burundi utasaidia kujua idadi kamili ya wakimbizi hao waliotoroka nchini humo miaka 3 iliyopita. Awali walikadirika kuwa elfu 84,idadi ambayo pande mbili zinasema imebadilika kwa sasa. Add a comment

Kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya uliofanyika October 2017, na kuleta mkanganyiko mkubwa wa kisiasa nchini humo, Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani wa NASA Raila Odinga leo March 9, 2018 wamekutana rasmi na kuzungumza.

Add a comment
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza watu anaopendekeza waidhinishwe kuwa mawaziri katika serikali yake mpya baada yake kushinda uchaguzi mwaka jana. Mawaziri sita ambao walikuwa wanahudumu katika serikali yake muhula uliopita wamevuliwa uwaziri na kuteuliwa kuwa mabalozi. Add a comment

Zaidi ya madaktari 500 katika hospitali kuu ya Kenyatta nchini Kenya wamesusia kazi wakitaka kurejeshwa kwa mwenzao aliyesimamishwa kazi baada ya kumfanyia kimakosa mgonjwa upasuaji wa kichwa. Kadhalika wanadai marupurupu ambayo wanasema hawajalipwa. Mwenyekiti wa Muungano wa Madaktari nchini, Samuel Oroko, amesema kumsimamisha kazi daktari huyo ilikuwa ni uamuzi ambao hauwezi kutatatua shida zinazoikumba hospitali hiyo.

Add a comment

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, limezindua uuzaji wa tiketi za safari ya kwanza kabisa ya ndege zake za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi Marekani.

Add a comment
Wakili maarufu wa Haki za Binadamu Haron Ndubi ambaye amefikishwa Mahakamani asubuhi ya leo February 12, 2018. Wakili Ndubi amefikishwa Mahakamani baada ya kubishana na Maaskari wa barabarani baada ya kukataa kufuata maelekezo aliyopewa na askari hao, tukio ambalo limetokea katika Barabara ya Jakaya Kikwete. Inaelezwa kuwa Maaskari hao walimwagiza kupumua kwenye kifaa maalumu cha kupima dereva ana kiwango gani cha pombe mwilini kutokana na kuhisi kuwa Wakili huyo alikuwa akiendesha gari akiwa amelewa. Hata hivyo ameachiwa kwa dhamana ya Ksh 30000 sawa na Tshs 67000. Add a comment

Ulinzi umeimarishwa katika jiji kuu la Kenya, Nairobi pamoja na miji mingine mikuu Rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kuapishwa kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine hapo kesho.

Add a comment

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.