Star Tv

Mbunge mmoja wa Kenya amekamatwa kufuatia matamshi aliyotoa dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wikendi iliyopita, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Johanna Ng’eno anatuhumiwa kwa kutumia maneno ya matusi kumdhalilisha rais, kulingana na taarifa ya gazeti la Daily Nation inayonukuu ripoti ya polisi.

Kanda ya video inayomuonesha mbunge huyo akizungumzia mgogoro kati ya rais Kenyata na naibu wake William Ruto imezua gumzo kali katika mitandao ya kijamii.

Mbunge huyo alisikika akimwambia Rais avunje serikali ikiwa ameshindwa kufanya kazi na Bwana Ruto.

Aidha, hali ya taharuki ilishuhudiwa wakati wa kukamatwa kwa mbunge huyo wa Emurua Dikirr, katika eneo la bonde la ufa huku tukio hilo likioneshwa moja kwa moja katika ukurasa wake wa Facebook.

Baada ya kukamatwa kwa bwana Ng'eno, Naibu wa Rais aliandika ujumbe katika Twitter yake akisema "viongozi wanapaswa kujizuia na kuepuka kutumia lugha ya matusi dhidi ya Wakenya wengine".

CHANZO:BBC Swahili.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.