Star Tv

Muungano wa wanahabari nchini Burundi, umetoa wito kwa rais Évariste Ndayishimiye kuwasamehe wanahabari wanne wa Gazeti binafsi la Iwacu, waliofungwa jela kwa kosa la kutishia usalama wa nchi hiyo.

Waandishi hao walishtumiwa kosa hilo walipokwenda kuripoti mapigano kati ya wanajeshi na kundi lenye silaha, katika Mkoa wa Bubanza mwaka uliopita.

Mapema mwezi Juni mwaka huu Mahakama ya Rufaa nchini Burundi ilipitisha hukumu ya miaka miwili iliyotolewa kwa waandishi hao ambao walikuwa walihukumiwa katika mahakama ya mwanzo kwa makosa ya kuhatarisha usalama wa taifa.

Waandishi hao ni wafanyakazi wa shirika la habari la Iwacu ambalo ni moja kati ya mashirika machache binafsi katika taifa hilo.

Waandishi hao wanne waliohukumiwa, walikamatwa mnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita katika eneo la Musigati, mkoani Bubanza, huku vituo kadhaa vya redio na vyombo vingine vya habari vilifungwa na waandishi wengi wa habari waliikimbia nchi hiyo.

Kamati ya Kuwalinda Wanahabari (CPJ) na mashirika mengine 80 ya kutetea haki za wanahabari na haki za kibinadamu hivi majuzi walituma barua kwa viongozi wa nchi za Afrika, kuwahimiza kuwaachia huru wanahabari wote wanaozuiliwa kwa kuzingatia mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19.

 

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.