Star Tv

Wizara ya Afya nchini Kenya imetangaza ongezeko la wagonjwa wapya wa corona 28, na wagonjwa hao ni waliopimwa ndani ya saa 24.

Wagonjwa hao wapya walioripotiwa leo Katibu wa Wizara ya Afya Rashid Aman wameifanya idadi ya wagonjwa nchini humo kufikia 700 kutokea wagonjwa 672 ambao walioripotiwa jana Jumapili Mei 10.

Bwana Rashid amesema kwamba kati ya wagonjwa hao wapya 10 wanatokea Mombasa , 9 wanatokea Kajiado na 7 wanatokea Nairobi huku 2 wakitokea Wajir.

Aidha,Wizara hiyo imeripoti uwepo wa kifo cha mgonjwa mmoja na kufanya waliofariki kwa ugonjwa huo mpaka sasa kufikia 23, huku watu 12 wameripotiwa kupona na kufanya idadi ya waliopona kufikia 251.

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.