Star Tv

Kenya imeripoti jumla ya visa 411 vya maambukizi ya virusi vya corona Ijumaa ya leo Aprili 01,Mei,2020.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa nchi hiyo Bwana Mutahi Kagwe amesema kuwa watu 15 zaidi wamepatikana na virusi bya corona kufuatia uchunguzi wa vipimo vya sampuli 1,434 vilivyofanywa saa 24 zilizopita.

Kenya ambayo ilithibitisha kupata maambukizi ya kwanza ya corona mwezi Machi, imekwishapima sampuli 21,702 kutoka maeneo mbali mbali ya nchi hadi kufikia tarehe 1 Mei.

Waziri huyo wa afya amesema kuwa idadi ya watu waliopona virusi vya corona imepanda na kufikia watu 150 huku sita zaidi wakiruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupona.

Wizara hiyo imesema kuwa idadi ya vifo vilivyosababishwa na Covid-19 imefikia watu 21 baada ya wagonjwa 4 zaidi kufariki dunia.
Kufuatia kutangazwa kwa upimaji wa jumla katika maeneo ya nchi, Wizara imefanya shughuli hiyo katika eneo lenye msongamano wa watu wengi la Kawangware jijini Nairobi siku ya Ijumaa.

Lengo la shughuli hiyo ni kuwabaini na kuwatenga watu walioambukizwa na kutafuta watu waliokutana nao ili kuzuwia kusambaa zaidi kwa virusi vya corona.

Wizara ya Afya na huduma za umma imesema itaanzisha hazina ya kuwasaidia wafanyakazi wa Afya wanaokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona huku Wizara ya elimu imesema itachukua hatua kuwalinda wanafunzi kutokana na athari mbaya za hatua zilizochukuliwa kukabiliana na Covid-19.

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.