Star Tv

Wizara ya Afya nchini Kenya imetangaza ongezeko la wagonjwa 15 wapya waliothibitishwa kuwa na virusi vya corona na kufanya wagonjwa waliopata maambukizi ya Corona nchini humo kufikia 296.

Wagonjwa 11 ni raia wa Kenya na wanne ni raia wa kigeni ambao walikuwa miongoni mwa watu 545 waliofanyiwa vipimo vya kubaini ikiwa wana virusi vya ugonjwa huo katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Akizungumza na wanahabari Jumanne Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mercy Mwangangi amesema visa saba vya maambukizi vilirekodiwa Mombasa pwani ya Kenya, sita mjini Nairobi na viwili katika mji wa kaskazini mashariki wa Mandera.

Pia Dkt. Mwangangi amesema hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa amesafiri na kuongeza kuwa watu sita kati yao walikuwa karantini na wengine tisa walipatikana kupitia mkakati wa serikali wa kuwatafuta watu wanaoshukiwa kuambukizwa baada ya kuchangamana na watu walioathirika.

Dkt. Mwangangi pia alitangaza kuwa watu watano zaidi wametolewa hospitali baada ya kupona na kuongeza idadi ya watu waliopona kutokana na virusi vya corona nchini humo kufikia 74.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.