Star Tv

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi kufikia 281 baada ya visa vingine 11 kuthibitishwa leo Jumatatu.

Kati ya wagonjwa hao 11 watano kati yao ni wanawake na wanaume 6, Wagonjwa wote wana umri kati ya miaka 11-80.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema wagonjwa wapya saba wameripotiwa mjini Mombasa Pwani ya Kenya huku wanne wakitokea jijini Nairobi.
Wagonjwa wawili wamepona na kuruhusiwa kuenda nyumbani na kuongeza idadi ya waliopona ugonjwa huo nchini Kenya kufikia 69.

Waziri Kagwe pia amethibitisha kuwa jumla ya watu 455 wamekamatwa na kuwekwa karantini ya lazima kwa kukiuka masharti ya kafyu iliyowekwa kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Serikali ilikuwa imetoa onyo kwamba watakaokiuka watawekwa karantini ya lazima kwa gharama yao baada ya visa vya watu kukamatwa kwenye baa na hafla za nyumbani kuongezeka.

Pia kumekuwa na madai ya watu kutoa hongo kwa polisi ili kupita vizuizi na kuingia au kutoka miji iliyowekewa marufuku ya usafiri kama vile Nairobi.

Kenya ina jumla ya vituo 33 vya karantini vinavyowazuilia watu 483 kwa sasa, huku vifo vilivyotokana na ugonjwa wa corona nchini humo bado ni 14.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.