Star Tv
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza watu anaopendekeza waidhinishwe kuwa mawaziri katika serikali yake mpya baada yake kushinda uchaguzi mwaka jana. Mawaziri sita ambao walikuwa wanahudumu katika serikali yake muhula uliopita wamevuliwa uwaziri na kuteuliwa kuwa mabalozi. Bw Dan Kazungu, ambaye amekuwa waziri wa madini, amependekezwa kuwa balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania. Aliyekuwa balozi wa Kenya nchini humo Chirau Ali Mwakwere alijiuzulu mwaka jana ili kuwania kiti cha ugavana katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti. Alishindwa kwenye uchaguzi huo.Miongoni mwa walioteuliwa kuwa mawaziri wapya ni mwanahabari mkongwe Farida Karoney ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa ardhi. Wadhifa huo ulikuwa unashikiliwa na Prof Jacob Kaimenyi ambaye amependekezwa kuwa balozi wa Kenya katika Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Sayansi, Elimu na Utamaduni (Unesco) mjini Geneva. Bi Monica Juma ameteuliwa kuwa waziri mpya wa mambo ya nje kuchukua nafasi ya Amina Mohamed ambaye amependekezwa kuwa waziri wa elimu. Mawaziri walioteuliwa kuwa mabalozi Judi Wakhungu (Mazingira) - Ufaransa Cleopa Mailu (Afya) - Umoja wa Mataifa mjini Geneva Dan Kazungu (Madini) - Tanzania Phylis Kandie (Leba na Jumuiya ya Afrika Mashariki) - Ubelgiji, Luxemburg na Umoja wa Ulaya Willy Bett (Kilimo) - India Jacob Kaimenyi (Ardhi) -UNESCO, Paris Hassan Wario (Michezo) - Austria Kwa sasa, orodha kamili ya mawaziri waliopendekezwa ni: Adan Mohammed - Viwanda Amina Mohammed - Elimu Charles Keter - Kawi Eugene Wamalwa - Ugatuzi Farida Karoney - Ardhi Fred Matiangi - Masuala ya Ndani na Usalama Henry Rotich - Fedha (Hazina Kuu) James Macharia - Uchukuzi John Munyes - Madini na Mafuta Joseph Mucheru - Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Keriako Tobiko - Mazingira Margaret Kobia - Vijana na Utumishi wa Umma Monica Juma -Mambo ya Nje Mwangi Kiunjuri - Kilimo Najib Balala - Utalii Peter Munya - Jumuiya ya Afrika Mashariki Racheal Omamo - Ulinzi Raphel Tuju - Waziri (Bila wizara kwa sasa) Rashid Achesa - Michezo Sicily Kariuki - Afya Simon Chergui - Maji Ukur Yattany - Leba

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.