Star Tv

Ujumbe wa Waangalizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) nchini Kenya umeipongeza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kutekeleza zoezi la upigaji kura lililokamilika Jumanne.

Katika hotuba kwa wanahabari Alhamisi jijini Nairobi, ujumbe wa waangalizi ulisema kwamba polisi pia walikuwa katika nafasi ya kuhakikisha wapiga kura wanalindwa wakati wa zoezi hilo katika vituo vya kupigia kura.

Kiongozi wa ujumbe huo Jakaya Kikwete Rais wa zamani wa Tanzania amesema kuwa polisi hawakuingilia zoezi la upigaji kura.

"Ujumbe unaipongeza IEBC kwa kutumia vyema teknolojia katika usajili wa wapigakura, kuwatambua wapigakura na uwasilishaji wa matokeo,” - Kikwete.

Aidha Kikwete amesema teknolojia hiyo imeongeza ufanisi na kuongeza uwazi nchini, tofauti na chaguzi zilizopita.

Hata hivyo, Kikwete amebainisha kwamba kulikuwa na matukio machache yanayohusiana na utambulisho wa wapiga kura na kitengo cha KIEMS, akiomba tume kuzingatia masuala hayo na kutatua siku zijazo.

"Tunapendekeza kwamba matatizo yanayohusiana na vifaa vya KIEMS yatambuliwe na hatua muhimu za kurekebisha zichukuliwe kwa utendakazi bora katika siku zijazo."

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.