Star Tv

Mpiga mbizi ambaye amekuwa akisaidia kuopoa maiti kutoka Mto Yala magharibi mwa Kenya amejificha baada ya kutishiwa maisha yake, shirika la kutetea haki za binadamu linasema.

Mpiga mbizi huyo anasema amehusika katika kuopoa miili isiyopungua 25 tangu katikati mwa mwaka jana.

Wakati timu ya BBC ilipozuru eneo hilo katika kaunti ya Siaya mwezi uliopita, mzamiaji huyo alieleza jinsi baadhi ya maiti alizopata zikiwa zimefungwa viungo vyao pamoja, huku nyingine zikiwa kwenye magunia.

Wakati huo alisema baadhi ya maafisa wa polisi hawakufurahishwa na hatua ya yeye kuzungumza na wanaharakati wa haki za binadamu na waandishi wa habari kuhusu hali hiyo.

Alitakiwa asizungumze na vyombo vya habari na polisi pia wanapinga kauli zake, wakisema miili imegunduliwa kwa zaidi ya miaka miwili.

Shirika la Haki Africa linasema mwanamume huyo sasa ametishwa na polisi.

Mpiga mbizi huyo hivi majuzi aliitwa na polisi, akazuiliwa kwa saa nane na kunyanganywa simu yake, shirika hilo la kutetea haki za binadamu lilisema katika taarifa ya mkurugenzi wa Haki Africa Hussein Khalid ambapo aliiambia BBC kuwa, shirika hilo limeamua kumficha kwasababu ya wasiwasi wa ustawi wake.

Katika visa vyote viwili, wanaume hao walikuwa wameripotiwa kutoweka ndani ya miezi mitatu iliyopita na wote wawili walikuwa wameonekana mara ya mwisho wakiwa hai zaidi ya kilomita 200 (maili 124) kutoka Mto Yala, na kuzua maswali kuhusu jinsi walivyofika huko.

Aidha mashirika ya kutetea haki za binadamu yamehoji iwapo kuna uwezekano wowote wa polisi kuhusika katika vifo hivyo.

#ChanzoBBC

Latest News

Waziri Mkuu Akagua Visima Vya Dharura Dar Es Salaam
10 Nov 2022 13:31 - Kisali Shombe

¬†WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]

Waziri Wa Afya Aagiza Udhibiti Magonjwa Ya Mlipuko
09 Nov 2022 14:15 - Kisali Shombe

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum  [ ... ]

Vifo vitokanavyo na Utoaji wa Mimba usio salama, Kudhibitiwa
09 Nov 2022 13:21 - Kisali Shombe

Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.