Chama cha wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) chini ya mkurugenzi Mtendaji Wakili David Sigano kwa kushirikiana na baraza la habari Tanzania (MCT) waandaa mafunzo kwa waandishi wa habari.
Mafunzo haya ambayo yamefanyikia jijini Mwanza tarehe 16/08 ikiwa mwenyeji wa mafunzo haya ni Klabu ya waandishi wa Habari wa mkoa wa Mwanza (MPC) chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Edwin Soko. Mafunzo haya yakiwa na lengo la kuangalia changamoto na mwenendo a habari katika suala la uhuru wa habari, uhuru wa kujieleza, sanjari na uhuru wa vyombo vya habari, hali ya kupata taarifa na kufanya kazi katika ufanisi kwa waandishi wa habari, sambamba na majadiliano juu ya sheria za vyombo vya habari.
Mafunzo haya juu ya suala la sheria ikiwa ni mara ya kwanza kwa Chama cha wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) kutoa mafunzo kama haya kwa waandishi wa kanda ya ziwa.