Star Tv


Ofisi ya upelelezi ya Rwanda (RIB) imethibitisha kuwa inamshikilia Mkuu wa makasisi wa Kanisa katoliki Parokia ya Rwamagana nchini humo, Jean-Marie Telesphore Ingabire, ambaye anashukiwa kusaidia katika madai ya wizi na kuficha ushahidi.

Msemaji wa RIB Thierry Murangira, ameiambia BBC kuwa Padre Ingabiri amekamatwa na Mamilioni ya fedha yanayodaiwa kuwa ni ya wizi.

"Mkuu wa mapadri wa Parokia ya Rwamagana ya Kanisa Katoliki yuko mahabusu, anashutumiwa wa kusaidia katika madai mashitaka ya wizi, huku uchunguzi ukiendelea,”- amesema Murangira.

Uchunguzi bado unaendelea kubaini kiasi cha pesa kilichohusika, alisema Bw. Murangira na kuongeza kuwa kasisi huyo alikuwa akitunza pesa haramu zinazodaiwa kuibwa, jambo lililowafanya waendelee na wizi.

Vyanzo mbalimbali vinaonesha kuwa watu kadhaa walikamatwa tangu mwishoni mwa wiki iliyopita kwa tuhuma za wizi, akiwemo ndugu zake Padre Ingabire ambao walipatikana wakiwa wamejificha na kiwango kikubwa cha fedha.

Kasisi huyo anasemekana kushindwa kuelezea ni kwa vipi alikuwa na mamilioni ya fedha nyumbani kwake, wakati msako ulipofanyika kwenye makazi yake.

Aidha, Murangira amsema kuwa RIB inatarajia kupata maelezo zaidi wakati uchunguzi ukiendelea.
#ChanzoBBCSwahili

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.