Star Tv

Mkuu wa jeshi la UPDF Jenerali David Muhoozi ameomba msamaha kwa waandishi wa habari kufuatia tukio la jana wakati polisi wa jeshi la UPDF walipowatandika wandishi habari.

Waandishi wa habari hao walikuwa wakimsubiri kiongozi wa chama cha NUP Robert Kyagulanyi, aliyepeleka malalamiko yake kwenye Kamisheni ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa Kololo.

Jenerali David Muhoozi amesema uchunguzi umeanza kwa waliofanya kitendo hicho na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Jeshi hilo limesema litalipa gharama za matibabu ya wandishi habari hao.

Waandishi waliojeruhiwa ni Cliff Wamala wa NTV, Josephy Dhabiti NBC,Rashid Nakayi GalaxyFm, Timoth Murungi New Vision, Irene Abaro Monitor, Josephine Namakumbi NBS na Jeff Twesigye NTV.

Jenerali Muhoozi amesema jeshi la UPDF halikuwatuma wanajeshi hao kuwapiga waandishi wa habari.

Aidha, ametoa wito kwa waandishi habari kuwa na vitambulisho vinavyoonesha wakiwa kazini kusaidia kuwatambua na mwisho amesema watafanya mpango kuzungumuza na waandishi wa habari ili kuboresha mahusiano kati ya pande hizo mbili.

Chanzo na BBC Swahili.

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.