Star Tv

Watu 32 wamethibitishwa kufariki kwenye ajali ya gari nchini Uganda iliyotokea usiku wa kuamukia leo katika wilaya ya Kasese.

Vifo hivyo vimetokea baada ya magari matano kugongana katika kijiji cha Kihongo kilichopo kwenye barabara kuu ya Hima –Rugendabara wilayani Kasese magharibi mwa Uganda.

Miili ya marehemu 32 imepatikana na majeruhi watano wamepelekwa katika hospitali ya Kilembe.

Katika taarifa iliyotolewa na shirika la Msalaba mwekundu nchini humo, timu yao ikishirikiana na jeshi la UPDF na Polisi ikiongozwa na Meja Charles Nzei wameweza kuwaokoa majeruhi na kupata miili ya waliofariki.

Sababu ya ajali hiyo imetajwa kuwa ni ufinyu wa barabara inayotengenezwa na kulikuwa giza kubwa na hivyo kusababisha Malori mawili kugongana mjini Kasese na kuanguka.

Baada ya yaliangukakwa malori mawili ambayo tayari , gari lingine kutoka Budibugyo pia likaanguka kwenye katika eneo hilo hilo.

Kwa pamoja magari 5 yakaanguka kwanye ajali iliyosababaisha vifo vya watu 32 na watano kujeruhiwa vibaya majira ya saa tatu za usiku kwa mujibu wa msemaji wa Red Cross Irene Nakasita.

Kati ya magari hayo L ori dogo ya aina ya kenta lilikuwa limebeba jeneza na watu waliokuwa wakielekea kwenye mazishi wakitoka wilayani Budibugyo wakielekea Kata ya Maliba.

Kwa mujibu wa takwimu za jeshi la polisi nchini Uganda karibu ajali za barabarani 20,000 hutokea kila mwaka nchini Uganda na kusababisha takribani vifo vya watu 2,000.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.