Star Tv

Kenya inatarajia kupokea dozi milioni 24 za chanjo ya ugonjwa corona iliyotengenezwa na kapuni ya Astrazeneca na chuo kikuu cha Oxford mwezi ujao, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe nchini Kenya amesema kuwa chanjo hizo ziliagizwa kupitia mpango wa Umoja wa Afrika.

Waziri wa mambo ya nje Uingereza, Dominic Raab, ambaye yuko nchini humo kwa ziara ya siku moja, amenukuliwa akisema Uingereza ilikuwa inasaidia Kenya kujitayarisha kuanza kutoa chanjo hiyo.

"Ni wajibu wetu sio tu kimaadili, lakini ni kwa maslahi ya Uingereza kuona raia wa Kenya wakipata chanjo hiyo haraka iwezekanavyo kadri ya uwezo wetu," Bwana Raab amenukuliwa akisema.

Kenya ina idadi ya watu takriban milioni 48, kulingana na takwimu ya idadi ya watu mwaka 2019.

Na hadi kufikia sasa nchi hiyo imethibitisha maambukizi 99,308 ya virusi vya corona huku watu 1,130,707 wakifanyiwa vipimo vya virusi hivyo.

Pia, watu 82,478 wamethibitishwa kupona ugonjwa huo wa corona huku idadi ya vifo ikiwa 1,734.

 

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.