Star Tv

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Uganda, Jaji Simon Byakama ametangaza kuwa kuanzia leo mtu yeyote hatakiwi kufanya kampeni za namna yeyote ile.

Aidha amesema uchaguzi utafanyika kesho Januari 14,2021 siku ya Alhamis, huku kukiwa na jumla ya wapiga kura wa kiume ni zaidi ya milioni nane na wanawake wakiwa zaidi ya milioni tisa.

Bw Byakama amesisitiza pia kuwa waandishi wa habari hawataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha kupitia kura.

Wakati tume ya uchaguzi ikitoa tamko hilo, Inadaiwa kuwa watetezi wa haki za binadamu wanne wa Kenya wamekamatwa nje ya ubalozi wa Uganda jijini Nairobi asubuhi muda mfupi kabla ya kuwasilisha taarifa yao kwa vyombo vya habari kuhusiana na ukatili wa polisi dhidi ya upinzani nchini Uganda.

Wanaharakati hao ambao kwa sasa wanashikiliwa kwa ajili ya kuhojiwa na polisi ambao ni pamoja na Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika, Hussein Khalid pamoja na mwandishi wa habari Yassah Musa.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.