Star Tv

Mgombea wa urais kupitia chama cha upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu kama Bobi Wine amethibitisha kupeleka watoto wake nje ya nchi kwa kuhofia usalama wao.

Bobi Wine amesema taifa hilo linafahamu vyema changamoto ambazo familia yake imepitia tangu alipoamua kupambana na Rais aliye madarakani Yoweri Museveni katika uchaguzi mkuu unaofanyika Januari 14.

"Watoto wangu wameishi kwa hofu kwa kipndi cha miaka mitatu iliyopita....mara nyingi tu gari linalotufuatilia limekuwa likiwafuatilia na wao hata kwenda na kutoka shuleni’’- amesema Bobi Wine.

Bobi Wine pia amesema kuwa mwaka jana, gari lililokuwa linasafirisha watoto wake lilishambuliwa moja kwa moja jambo lililomfanya kuwabadilisha shule na kuimarisha usalama wao.

Kulingana na Bobi Wine kwa kipindi kirefu mwaka huu, watoto wake wameishi kama wafungwa ikiwa ni nadra sana wao kutoka nje ya nyumba yao.

Katika akaunti ya mtandao wake wa Facebook, Bobi Wine amesema kuwa amepokea taarifa za mipango ya kuwadhuru watoto wake.

‘’Mwaka 2017, usiku wa mdahalo, walimrushia kijana wangu gurunedi, kupitia dirisha la chumba chake cha kulala na kuacha ujumbe kwamba nijiondoe au matokeo nitayaona’’, amesema Bobi Wine.

Na kuongeza kuwa hiyo ndio sababu alipopokea taarifa za njama ya kumvamia yeye, mke wake na kutekwa nyara kwa watoto wake, rafiki zake nje ya nchi wamejitolea kukaa na familia yake kwa muda.

Bobi Wine amebainisha kuwa; "Haimaanisha kuwa mimi na mke wangu tuko salama kwa kusalia nyuma. Lakini juhudi zetu ni kuhakikisha kuwa hawapati fursa ya kuteka nyara watoto wetu na kuitumia kama njia ya kunitisha’’.

Bobi Wine amesema katika nchi yenye demokrasia hakuna anayestahili kuishi kwa hofu kwasababu tu anapinga serikali.

Vilevile, Bobi Wine ameonesha kutoridhishwa na kitendo alichodai kuwa mfanyakazi wa uhamiaji amevujisha taarifa za watoto wake kusafiri nje ya nchi.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.