Star Tv

Vyama vya upinzani nchini Uganda wameungana kuwa na kituo chao kimoja cha kuhesabu kura katika uchaguzi mkuu.

Vyama hivyo ni NUP, FDC, JEEMA, DP, ANT na mgombea wa kiti cha urais wa kujitegemea Jeneri Henery Tumukunde na Dk.Kiiza Besigye wa serikali ya wananchi

Jukwaa linalojulikana kama UID litahusisha matumizi ya teknolojia na nyenzo zingine kuhakikisha kuwa takwimu za matokeo ya uchaguzi kutoka sehemu mbalimbali nchini Uganda yanahakikiwa ipasavyo.

Hii ina maana kuwa wawakilishi wa vyama vyote vya kisiasa kwenye kituo watashirikiana katika kutoa taarifa kuhusu hali ilivyo kuanzia mwanzo hadi mwisho hasa wakifuatilia vitendo ya ukiukaji wa haki za binadamu.

Mwanasiasa mkongwe Paul Semwogerere aliyewahi kuwania kiti cha urais mwaka 1996 dhidi ya rais ndiye mratibu wa jukwaa hilo.

Daktari Kizza Besigye ambaye amewahi kugombea kiti cha urais mara nne na kushindwa na rais Museveni amenukuliwa akisema kwamba japokuwa upinzani ulishindwa kuungana kuwa na mgombea mmoja, muungano huu ni muhimu sana kuweza kukabiliana na jaribio lolote la wizi wa kura.

Mwenyekiti wa chama cha Jeema ameeleza kuwa wameamua kuwa na kituo chao kwasababu tayari chama tawala cha NRM kimetangaza kuwa watakuwa na kituo chao tofauti na tume ya uchaguzi lakini wenye kutangaza matokeo ni tume ya uchaguzi.

Latest News

WANAOGESHA MAGARI BARABARANI HOVYO KUWAJIBISHWA BILA HURUMA.
20 Jan 2021 14:26 - Grace Melleor

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ameitaka Bodi ya mfuko wa Barabara (RfB) kutumia vifungu [ ... ]

KENYA KUPOKEA DOZI MILIONI 24 ZA CHANJO YA CORONA.
20 Jan 2021 14:06 - Grace Melleor

Kenya inatarajia kupokea dozi milioni 24 za chanjo ya ugonjwa corona iliyotengenezwa na kapuni ya Astrazeneca na chuo ki [ ... ]

BIDEN AJIANDAA KUINGIA IKULU, HUKU TRUMP AKISUSIA KUHUDHURIA KUAPISHWA KWAKE.
20 Jan 2021 08:14 - Grace Melleor

Rais mteule wa Marekani Joe Biden aliwasili Washington katika mkesha wa sherehe ya kuapishwa kwake, wakati mtangulizi wa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.