Star Tv


Serikali ya Rwanda imepiga marufuku usafiri wa umma na wa kibinafsi kati ya wilaya na mji mkuu wa Kigali.

Serikali ya nchi hiyo imetoa katazo hilo na kubainisha kwamba ni kutokana na hali ya kutisha ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Katika wiki moja tu Rwanda ilirekodi watu 30 waliokufa kutokana na ugonjwa huo.

Kulingana na kikao cha baraza la mawaziri hatua ya kupiga marufuku usafiri wa umma na kibinafsi kati ya wilaya na mji mkuu Kigali inaanza kutekelezwa leo.

Aidha, Hii ni mojawapo ya mikakati iliyochukuliwa kudhibiti wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona nchini Rwanda.

Serikali ya nchi hiyo imesema hali imekuwa mbaya na ya kutisha kutokana na kuongezeka sana kwa visa vya maambukizi pamoja na vifo vya watu.

Takwimu zinazotolewa na maafisa wa afya wa Rwanda zinaonyesha kwamba jumla ya watu 105 wameshafariki dunia kutokana na Covid 19 ambapo nusu yao walipoteza maisha mnamo Desemba tu.

Akizungumza na Radio ya taifa, Daktari Tharcisse Mpunga anayesimamia huduma ya msingi ya afya alieleza kwamba "katika kiwango hiki nchi inapaswa kutekeleza sheria ya kutotoka nyumbani kote nchini...lakini hatukupenda maisha yasimame kabisa’’.

Dr Mpunga ameongeza kwamba hali ilivyo sasa wagonjwa mahtuti wanakufa haraka sana pamoja na watu wa rika mbalimbali wakiwemo pia vijana.

Katika hatua mpya zilizotangazwa jana usiku wa manane, biashara zote ziliamriwa kufungwa saa kumi na mbili jioni.

Mikusanyiko yote ya kijamii na hafla nchini humo ni marufuku, na amri ya kutotoka nje kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi alfajiri imebaki.

Kadhalika imetangazwa kwamba watalii wa ndani na wa kimataifa wanaweza kusafiri kote nchini lakini baada ya kupima covid 19 na kuthibitisha kuwa hawana maambukizi ya ugonjwa huo.

Maafisa wa Afya wa Rwanda wanaamini kuwa ongezeko la maambukizi huenda lilichangiwa na sikukuu za Chrismass na mwaka mpya ambapo watu walisafiri sana kwenda maeneo yao asilia.

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.