Star Tv

Ofisi ya chama cha mgombea wa Urais nchini Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi imevamiwa na makumi ya wanajeshi wenye silaha pamoja na maafisa wa polisi.

Kutokana na uvamizi huo uliofanyanywa na wanajeshi wa nchini humo, nyaraka zimeripotiwa kuchukuliwa kutoka kwenye ofisi  ya mwanasiasa huyo ikiwa ni pamoja na kofia yenye muundo wa kijeshi na magwanda.

Mmoja wa washauri wa Bobi ameliambia shirika la BBC kuwa maafisa hawakuwasilisha kibali walipokua wakiingia kukusanya nyaraka na mavazi.

Msemaji wa polisi nchini Uganda Fred Enanga ameliambia shirika la utangazaji la BBC; “tunafanya operesheni juu ya utumiaji mbaya wa sare za kijeshi”.

Septemba mwaka jana, serikali iliidhinisha kofia nyekundu sawa na anayovaa Bobi Wine na wafuasi wake ni sare ya jeshi-ikimaanisha kuwa yeyote anayeonekana ameimiliki au kuivaa kinyume cha sheria anaweza kushitakiwa.

Bwana Enanga amesema operesheni inaendelea na kwamba maafisa watasaka maeneo mengine pamoja na ofisi za National Unity.

Bobi Wine amesema kuwa nguvu za dola zinamlenga na chama chake wakati akijiandaa kukabiliana na Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi ujao wa mwaka 2021, lakini msemaji wa polisi anasisitiza kuwa operesheni hiyo haijachochewa kisiasa.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.