Star Tv

Tume ya Mawasiliano ya Uganda ilitangaza wiki iliyopita ikieleza kuwa kuanzia sasa mtu yeyote anayechapisha maudhui mtandaoni atalazimika kujiandikisha kabla ya Oktoba 5,2020.

Kwa kutetea azimio hilo jipya, Tume ya Mawasiliano ya Uganda imetaja kifungu cha mamlaka ya Sheria ya Mawasiliano ya Uganda (Uganda Communication Act), ambayo inapiga marufuku uchapishaji wa maudhui bila kibali, Sheria ambayo itatumika kwa machapisho ya maudhui mtandaoni na kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa upande wa Roland Ebole, mmoja wa watafiti wa Shirika lisilo la kiserikali la Amnesty International amesema hiki ni kizuizi kingine kikubwa kuhusu uhuru wa kujieleza nchinihumo.

Kulingana na Roland Ebole ameeleza kuwa Waganda wote watalazimika kufuata kanuni hiiyo mpya, hatua hiyo inatia wasiwasi zaidi ikiwa imesalia miezi michache tu kabla ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka ujao.

Mtafiti wa Amnesty ameendelea kubainisha kuwa huenda tume hiyo imelenga kuwadhibiti wapinzani nchini humo; "Mikusanyiko yote ya kisiasa wakati wa kampeni ni marufuku, kwa hivyo wakati kuna vizuizi kuhusu njia za mawasiliano na habari, wakati ambapo serikali inakataza mikusanyiko ya umma, tunaweza fikiria kuwa lengo la mchakato huu ni kuzuia upinzani. "

Itakumbukwa kwamba mwanzoni mwa mwaka huu, mwezi Juni, tume ya uchaguzi ilitoa maagizo mapya, ambayo ni kama muongozo uliorekebishwa kwa uchaguzi wa mwaka 2021, na ambao unataka mchakato mzima wa uchaguzi ufanyike mtandaoni.

Chanzo: rfi Swahili.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.