Star Tv

Mtoto aitwaye Veronica Anthony mwenye umri wa miaka 17,Mwanafunzi wa darasa la saba wa Shule ya msingi Kayenze ambaye ni mkazi wa Iseni amefariki dunia kwa kupigwa na kitu kizito kichwani.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Muliro Jumanne Muliro, ametoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo Septemba 10,2020, Ambapo amebainisha kuwa;
"Tarehe 08.09 2020 Majira ya saa nne usiku maeneo ya Kata ya Kayenze wilayani Ilemela baba alimuua binti yake kwa kumpiga na kitu kizito kichwani kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani, kitendo kilichomkasrisha baba yake mzazi".

Aidha, Kamanda Muliro amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa uchunguzi wa Daktari, huku mtuhumiwa ambaye ni baba mzazi aliyejulikana kwa jina la Constatine Maningu tayari amekamatwa na atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.