Star Tv

Jeshi la Marekani limetangaza limefikia hatua ya kupunguza idadi ya wanajeshi wake waliopelekwa nchini Iraq, ambapo idadi ya wanajeshi itashuka kutoka kwa wanajeshi 5,200 hadi 3,000 ifikapo mwisho wa mwezi huu.

Shirika la habari la Reuters liliripoti mwezi uliopita kwamba Marekani itapunguza idadi ya wanajeshi wake nchini Iraq kwa karibu theluthi moja, Ambapo urasimishaji huu ulikuwa ukitarajiwa kwa muda mrefu.

Aidha, Wachambuzi wanachambuzi wa masuala ya usalama kutoka nchi tofauti wanaona kwamba vikosi vya Marekani vilivyopelekwa nchini Iraq vinachangia katika vita dhidi ya kundi la Islamic State (IS) lakini viongozi wa muungano wa kimataifa wanachukulia kuwa vikosi vya Iraq sasa vinaweza kudhibiti tishio hili peke yao.

"Tunaendelea kukuza mipango yetu ya ushirikiano ambayo inaimarisha vikosi vya Iraq na kutuwezesha kupunguza uwepo wetu nchini Iraq," amesema Jenerali wa kikosi cha majini Frank McKenzie, wakati wa ziara yake nchini Iraq.

Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye atawania katika uchaguzi wa urais wa Novemba 3, alifanya kampeni mwaka 2016 akiahidi kukomesha "vita visivyo na mwisho" vya Marekani, ambayo inaendelea kupunguza idadi ya wanajeshi wake katika nchi kama Afghanistan, Iraq na Syria.

Chanzo: rfi Swahili.

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.