Star Tv

Msemaji wa jeshi la Polisi nchini SACP David Misime amesema hali ya usalama na usimamizi wa ulinzi katika kampeni zinazoendelea nchini ni shwari na unaendelea vizuri.

Amesema Jeshi la Polisi limejiandaa vizuri katika kukabiliana na matishio ya aina yoyote ya kiusalama ambapo ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya nchi ili kuhakikisha kampeni za uchaguzi mkuu zinafanyika kwa amani na utulivu.

Aidha, Kamanda Misime amewatahadharisha wananchi, viongozi wa kisiasa pamoja na wadau wengine wa uchaguzi kuendelea kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria za nchi.

Misime ametoa onyo kwa watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii na ikiwa itatokea baadhi ya watu wamefanya mambo yatakayopelekea uvunjifu wa amani na usalama wa nchi watawajibishwa ipasavyo.

Jeshi la Polisi limesema liko imara kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama nchini inaendelea kuwa shwari hususani katika kipindi hiki ambacho kampeni zinaendelea, Ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza Uchaguzi Mkuu kufanyika siku ya Jumatano Octoba 28, 2020.

 

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.