Star Tv

Mwanamume mmoja ambaye ana umri wa miaka zaidi ya 80 nchini Ufaransa, ameilipua sehemu ya nyumba yake wakati alipokuwa akijaribu kumuua nzi.

Imeelezezwa kuwa mwanamume huyo alikuwa anakaribia kula chakula chake cha jioni na alikasirishwa na kelele ya nzi aliyekuwa anamzunguka.

Mwanamume huyo aliamua kuchukua kifaa cha umeme kilichotengenezwa kwa ajili ya kuwaua mende akaanza kumuua nzi huyo lakini kwa bahati mbaya gesi ilikuwa inavuja katika nyumba iliyopo kando ya mto Dordogne nchini Ufaransa.

Aidha, gesi na kifaa chake vilisababisha mlipuko na sehemu ya paa la nyumba yake iliyopo katika kijiji cha Parcoul-Chenaud kuharibika.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari nchini humo, mwanaume huyo ambaye hakuwa na silaha alibahatika kutoroka akiwa ameungua tu kwenye mkono wake.

Hata hivyo hatma ya nzi huyo aliyekuwa akimsumbua bado haijajulikana chombo cha habari cha Sud-quest kilisema.

Mwanaume huyo kwa sasa amejihifadhi katika hoteli moja ya eneo hilo huku familia yake ikikarabati nyumba yake.

Mwisho.

Credits: BBC Swahili.

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.