Star Tv

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofanya kampeni za kuharibu jina la nchi hiyo.

Hatua hiyo ya tamko la Rais Mnangagwa imemulikwa na kukosolewa vikali na wanaharakati wa haki za binadamu.

Hii inakuja siku kadhaa baada ya Rais Emmerson Mnangagwa kuvishutumu vyama vya upinzani kwa kushirikiana na mabalozi wa nchi za Magharibi kuhujumu uchumi na kuchochea vitendo vya kigaidi.

Wakati huo huo shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch limezitolea mwito nchi za Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC, kukemea hadharani ukandamizaji uliofanywa na serikali ya Zimbabwe dhidi ya maandamano ya amani ya kupinga ufisadi yaliyofanyika Julai 31.

Shirika hilo pia limelaani kamatakamata ya kiholela dhidi ya wapinzani nchini humo.

Katika ripoti yake iliyochapishwa wiki hii, Human Rights Watch inasema kuwa serikali ya Zimbabwe imewakamata kuhusiana na maandamanano hayo, watu wasiopungua 60, ikiwa ni pamoja na mwandishi wa vitabu Tsitsi Dangarembga na msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha Movement for Democratic Change, MDC Fadzayi Mahere.

Baada ya ripoti hiyo ya Human Right Watch inayoorodhesha visa vya kuwakamata kinyume cha sheria wakosoaji wa serikali nchini Zimbabwe, wakiwemo mwandishi wa habari aliyetuzwa kwa kazi yake Hopewell Chin'ono, na kiongozi wa kundi la kisiasa linalotaka mabadiliko la Transform Zimbabwe, Jacob Ngarivhume Rais wa nchi hiyo akatoa tamko la kusema kuwa sheria itapitishwa ambayo itatoa adhabu kali kwa wanaochafua taifa hilo.

Latest News

MIILI YA WATOTO 10 WALIOFARIKI KWA AJALI YA MOTO KYERWA YAAGWA LEO.
18 Sep 2020 10:38 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt.Bashiru Ally ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga miili 10 ya wanafunzi waliofar [ ... ]

“MSAIDIZI WA BENARD MEMBE HAJATEKWA, ANASHIKILIWA NA POLISI” –-KAMAMDA MAMBOSASA...
17 Sep 2020 12:58 - Grace Melleor

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema Jerome Luanda ambaye ni msaidizi wa Bernard  [ ... ]

WAZIRI MKUU WA LIBYA KUACHIA NGAZI MWISHONI MWA OKTOBA MWAKA HUU.
17 Sep 2020 12:30 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Libya Fayez el-Sarraj ametangaza kuachia wadhfa wake wa uwaziri mkuu mwishoni mwa mwezi Oktoba 2020.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.