Rais Trump ametoa wito kuwa uchaguzi wa Urais utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu uahirishwe kwa madai ya kuongezeka kwa upigaji kura kwa njia ya posta kunaweza kusababisha udanganyifu na matokeo yasiyo sahihi.
Rais Trump amekuwa akipinga upigaji kura kwa njia ya Posta ambao anadai unaweza kusababisha udanganyifu kwenye kura, ambapo kupitia ujumbe wake kwa njia ya Twitter ameandika "Kupiga kura kwa njia ya Posta kutafanya uchaguzi wa Novemba kuwa sio sahihi na wenye udanganyifu mkubwa katika historia ya nchi hiyo na aibu kubwa kwa Marekani".
Aidha, majimbo ya Marekani yanataka upigaji kura kwa njia ya Posta kufanywa kuwa rahisi zaidi kwasababu ya wasiwasi wa kwa matatizo ya kiafya kutokana na janga la corona.